Waziri wa Ujenzi, John Magufuli. |
Waziri
wa Ujenzi, John Magufuli ameupongeza Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) kwa
kuwachukulia hatua watendaji wa Kampuni ya Dott Services kwa kosa la
kuchelewesha ujenzi wa barabara ya Mkumbara hadi Same yenye urefu wa kilomita
96.
Kampuni
hiyo yenye makao yake makuu nchini Uganda, imeshindwa kukamilisha ujenzi wa
barabara hiyo unaogharimu Sh103.8 bilioni huku kampuni ya Strabag iliyochukua
ukandarasi wa kujenga barabara kama hiyo ya Korogwe hadi Mkumbara, ikimaliza
kazi yake Desemba 3, mwaka jana kama ilivyosaini mkataba.
Dk
Magufuli alitoa pongezi hizo wakati akikagua barabara hizo baada ya Mtendaji
Mkuu wa Tanroad, Patrick Mfugale kuelezea kwamba alilazimika kuwafukuza baadhi
ya mameneja wa Kampuni ya Dott Services wanaodaiwa kusababisha isikamilike kwa
wakati.
Alisema
kampuni hiyo ilishalipwa Sh44.5 bilioni za awali kama mkataba unavyoelekeza na
kutakiwa kukamilisha ujenzi kwa asilimia 67 kabla ya kulipwa fedha zingine.
Hata
hivyo, Mfugale alisema Kampuni ya Strabag iliyojenga barabara ya Korogwe hadi
Mkumbara yenye urefu wa kilomita 76 kwa Sh87.8 bilioni, imeishakabidhi na
kwasasa iko chini ya uangalizi hadi Desemba, mwaka huu. “Barabara hii iko chini
ya uangalizi hadi Desemba, mwaka huu, tunalenga kubaini kama kuna upungufu
uweze kurekebishwa,” alisema Mfugale.
Source: Mwananchi News
Post a Comment