Viongozi wakuu wa CCM Taifa. |
Kamati
Kuu ya CCM (CC) inakutana Jumamosi Februari 28, 2015 huku mambo muhimu sita yakitarajiwa
kujadiliwa, likiwamo suala la makada wa chama hicho waliopewa adhabu ya onyo
kali kwa kuanza kampeni za urais mapema na ukiukaji wa maadili.
Taarifa
kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,
Nape Nnauye, licha ya kutoeleza ajenda za kikao hicho, ilisema kitafanyika
jijini Dar es Salaam na kuongozwa na mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete
kuanzia saa 4 asubuhi.
Kikao
hicho kinafanyika wakati upepo wa kisiasa ndani ya chama hicho ukiwa haujatulia
huku kukiwapo masuala mazito ya kitaifa yanayotikisa medani za kisiasa,
likiwamo suala la uandikishaji wapiga kura, maandalizi ya kura ya maoni za
kupitisha Katiba Inayopendekezwa na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba,
ambayo yameelezwa na wachambuzi wa siasa kuwa hayawezi kukwepeka katika kikao
hicho.
Adhabu kwa wagombea:
Itakumbukwa
kuwa kikao hicho kitafanyika ikiwa ni siku 10 baada ya kukamilika tarehe ya
mwisho ya adhabu kwa makada sita wa CCM, waliokuwa wakitumikia adhabu ya miezi
12 kwa ukiukwaji wa maadili kwenye mchakato wa kutaka kuteuliwa na CCM kugombea
urais.
Kikao
kilichopita cha CC kilichoketi Januari 13, mwaka huu kilibainisha kuwa baada ya
muda wa adhabu zao kuisha, Kamati Kuu ingefanya tathimini kuona iwapo wagombea
hao walizingatia masharti ya adhabu zao na endapo kungekuwa na ambao
hawakuzingatia masharti adhabu zao zingeongezwa.
Wiki
iliyopita, Nnauye alithibitisha kuwa muda wa adhabu hiyo ulikuwa ukingoni na
kuwa viongozi hao wangefanyiwa tathmini na kamati ndogo ya maadili ili kubaini
iwapo adhabu hiyo ilitekelezwa ipasavyo.
Makada
waliokuwa wakitumikia adhabu hiyo ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa,
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Waziri
mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.
Post a Comment