Miezi minne iliyopita, Demeteriya Nabire
aliliwa na mamba alipokwenda mtoni karibu na makazi yake kuchota maji. Mnyama
huyu alirudi tena baaae katika eneo lilelile na kumkuta mume wa Nabire
anasubiri, tayari kwa kulipa kisasi.
Mumewe, Mubarak Batambuze, aliingiwa na hofu
sana, Nabire alikuwa mjamzito.hivyo Mubarak hakupoteza mkewe tu bali kiumbe
kilichokuwa tumboni.alijihisi kukosa nguvu, lakini Mwezi uliopita akasikia kuwa
Mamba amerejea.
''Mtu mmoja akaniita 'mubarak nina habari kwa
ajili yako, Mamba aliyemchukua mkeo amerudi, tena'
Mvuvi huyo mwenye umri wa miaka 50 akaelekea
mtoni na marafiki zake.'' alikuwa mkubwa, na tulijaribu kupambana nae kwa mawe
na fimbo lakini hatukufanikiwa,'' alisema.
Hivyo Batambuze alienda nyumbani kwa muhunzi.
''Nikamweleza kuwa napambana na Mamba ambaye
amenichukulia mke wangu na mtoto aliyekuwa tumboni.ninataka sana kulipa
kisasi, kisha nikamwambia anitengenezee silaha ambayo ingeweza kumuua mamba
huyo.
Mtu huyo alitaka nilipe kiasi cha pauni 3.20
ili atengeneze Mkuki.
Akiwa na mkuki wake mkononi alielekea kwenye
mapambano.
Lakini alipofika kwenye maji, Mamba alikuwepo
eneo hilo, lakini Marafiki wa Batambuze waliingiwa hofu na kumsihi
asimshambulie kwa kuwa alionekana mkubwa sana na angeweza kumla, wakamwambia
kuwa Mkuki huo hautafaa.
Batambuze akasisitiza waendelee kubaki,
''nilishindwa kumuua mwanzo, alisema,'' sioni tatizo nikifa wakati namuua Mamba
natatumia mkuki huu, na nitahakikisha amekufa''.
Ofisa wa wanyama pori Oswald Tumanya, amesema kuwa Mamba alikuwa na urefu wa zaidi
ya mita nne na uzito wa kilo 600.
''nilikuwa na wasiwasi sana lakini
kilichonisaidia ni Mkuki, '' alisema Batambuze.
Alifunga kamba kwenye kwenye mkuki kwenye
sehemu iliyotengenezwa mithili ya kisu kikali, ''niliweka silaha yangu eneo
Mamba alipo huku marafiki zangu wakinisaidia kurusha mawe na kumchapa mamba
mgongoni kwake wakitumia fimbo, Alijaribu kunyanyua mdomo wake juu ili
anishambulie.''
Ilichukua saa moja na nusu mwa Batambuze na
marafiki zake wakipambana na Mamba, hatimaye walifanikiwa kumuua.
Wakiwa wamechoka walirejea kijijini kwao
''kulikuwa na mshtuko mkubwa, kilichomshangaza kila mtu ni ukubwa wa Mamba,
hakuwa mamba wa kawaida, alikuwa mkubwa sana. Na Watu wakatuita mimi na
marafiki zangu mashujaa,'' alisema.
Chanzo: BBC News!
Post a Comment