Wabunge wa bunge la
Uingereza wameunga mkono sheria inayoruhusu uzaaji wa watoto wenye vinasaba,
DNA kutoka kwa wanawake wawili na mwaume mmoja, katika tukio la kihistoria.
Uingereza kwa sasa
itakuwa nchi ya kwanza kuweka sheria zinazoruhusu watoto wenye vinasaba vya
watu watatu tofauti.
Katika kura iliyopigwa
katika bunge la Commons, wabunge 382 waliunga mkono muswada huo wa sheria na
wabunge 128 walipinga mbinu inayozuia magonjwa ya kijenetiki kutoka kwa mama
kwenda kwa mtoto.
Wakati wa mjadala huo,
mawaziri wamesema mbinu hii ni "mwanga kwa safari ndefu ya giza" kwa
familia kupata watoto.
Upigaji kura zaidi
unahitajika katika baraza la bunge la juu, maarufu kama House of Lords. Iwapo
kila kitu kitakwenda sawa, basi mtoto wa kwanza wa teknolojia hii atazaliwa
mwaka ujao.
Watetezi wa mpango huu
wanasema uungwaji mkono wa sheria hii "ni habari njema kwa maendeleo ya
tiba" lakini wakosoaji wanasema wataendelea kupinga mpango huu ambao una
mashaka mengi kuhusu maadili na usalama katika uzazi huu.
Makisio yanasema watoto
150 wanaopatikana kutokana na vinasaba vya watu watatu watazaliwa kila mwaka.
Waziri Mkuu wa
Uingereza David Cameron anasema: "Hatuzungumzii Mungu hapa, tunahakikika
kuwa wazazi wawili ambao wanataka mtoto mwenye afya wanaweza kumpata."
Mpango huu ambao
umebuniwa Newcastle, utasaidia wanawake kama Sharon Bernardi, kutoka
Sunderland, ambaye alipoteza watoto wote saba kutokana na ugonjwa wa
mitochondrial.
Chanzo: BBC News!
Post a Comment