Kenya
intazamiwa kuanza kuuza mafuta ghafi ya petroli katika soko la kimataifa mwaka
ujao na hivyo kuitangualia nchi jirani ya Uganda ambayo iligundua bidhaa hiyo
miaka tisa iliyopita.
Ripoti
zinasema kuwa shirika la uchimbaji mafuta na gesi la Uingereza, Tullow
linatekeleza mkakati wa kuanza kuzalisha mafuta ya petroli katika eneo la
Lokichar kaskazini mwa Kenya.
Awali
shirika hilo lilikuwa limesema lingeanza kuuza nje mafuta ya Kenya mwaka 2018
lakini sasa limezidisha kasi ya uchimbaji wa mafuta na hivyo kutoa msukumo
mkubwa wa uchumi wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Shirika
la Tullow limesema linataraji bomba kutoka Lokichar hadi bandarini eneo la
pwani litakuwa tayari ili kuwezesha mafuta ghafi ya Kenya kufika katika soko la
kimataifa kabla ya kumalizika mwaka 2016.
Inatazamiwa
kuwa Kenya itaanza kwa kuuza mapipa laki moja ya mafuta ghafi ya petroli
ya siku. Kwa bei ya sasa ya dola 50 kwa pipa, nchi hiyo inaweza kupata pato la
takribani dola bilioni 1.825 au shilingi bilioni 166 kwa mwaka.
Kuanza
kuzalishwa mafuta ya Petroli mwisho wa mwaka 2016 kutasadifiana na wakati
ambao Wakenya watakuwa wakijirayarisha kwa uchaguzi wa mwaka 2017 na hivyo
mafanikio hayo yanatazamiwa kupigiwa debe na serikali ya Jubilee inayoongozwa
na Rais Uhuru Kenyatta.
BBC News
Post a Comment