Mjumbe wa Baraza la
Wawakilishi wa Jimbo la Mjini Mkongwe (CUF), Ismail Jussa (kulia) akiwa
amemnyanyua mkono juu kada wa Chama cha CUF, Mansoor Yussuf Himid walipokuwa
wakishiriki maandamano kuelekea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, mjini Unguja
jana. Picha na Edwin Mjwahuzi
CUF
kimeendelea kupeperusha bendera ya zamani ya chama cha Afro Shiraz Party (ASP),
ambacho kimefutwa kisheria baada ya kuungana na chama cha Tanu na kuzaliwa
Chama cha Mapinduzi(CCM), Februari 5, 1977.
Bendera
hiyo ya ASP ilipamba mkutano wa hadhara wa CUF uliofanyika jana kwenye uwanja
wa Mnazi Mmoja ambako chama hicho kilikuwa kinazindua rasmi kamati za uchaguzi
za chama hicho ambazo ni maalumu kwa ajili ya kushughulikia masuala yote
yanayohusu uchaguzi mkuu ujao ikiwa ni pamoja na maandalizi.
Tofauti
na ilivyozoeleka wafuasi wa chama hicho waliingia uwanjani hapo kwa makundi
huku karibu kila mmoja akiwa amebeba bendera ya ASP, yenye rangi tatu za
kijani, nyeusi na bluu bahari.
Kwa
mujibu wa taarifa wafuasi wa CUF wameanza utaratibu wa kupeperusha bendera ya
ASP kwa madai ya kuienzi Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), na pia kutanguliza
uzanzibari kwanza.
Hata
hivyo siku za karibuni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)
Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka aliiomba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini
kukichukulia hatua za kisheria chama cha CUF kwa madai ya kupeperusha bendera
ya zamani ya chama ASP kinyume na sheria namba 5 ya mwaka 1992.
Post a Comment