Kati
ya waliofariki wengi wao ni Mashabiki wa timu ya Zamalek ambao walifariki
kutokana na msongamano wakati Polisi walipowafyatulia mabomu ya machozi baadhi
ya mashabiki waliokuwa wakijaribu kuingia kwa nguvu ndani ya uwanja wakati timu
hiyo ilipokuwa ikipambana na timu ya ENPPI.
Mtandao
mmoja nchini humo uitwao AL-Misriyun umeripoti. Tukio hilo limetokea baada ya
Polisi kutumia gesi ya kutoa machozi kuwasambaratisha mashabiki walikokuwa
wakitumia nguvu kujaribu kuingia uwanjani.
Taarifa
ya Wizara ya mambo ya ndani ya Misri inasema kuwa Mashabiki wa Zamalek walikuwa
wanataka kuingia uwanjani kwa nguvu hivyo walikuwa wakiwazuia ili kunusuru mali
ya umma isiharibike.
Polisi
wamesema mashabiki hao walikuwa wanataka kuingia uwanjani bila tiketi,
wamenukuliwa wakisema Watu hao walipoteza maisha baadhi kutokana na msongamano
mkubwa wengine walipokuwa wakipambana na Polisi.
Ndani
ya uwanja kulionekana rundo la viatu karibu na miili ya Watu waliopoteza maisha
na wengine waliolala wakiwa majeruhi.
Mashabiki
wa Zamalek wanadai kuwa vurumai zilianza mamlaka ya uwanja ilipofungua Geti la
waya kuwaruhusu kuingia ndani.
Mashuhuda
wanasema uzio ulianguka wakati Watu walipokuwa wakipigania kuingia ndani hali
iliyosababisha msongamano mkubwa, mara askari wa usalama walianza kurusha
mabomu ya kutoa machozi.
Watu
walianza kukanyagana hali iliyosababisha Watu kupoteza maisha.
Tukio
hili limetokea ikiwa ni miaka mitatu tangu Wapenzi wa soka zaidi ya 70
walipopoteza maisha wakati vurugu zilipotokea katika uwanja wa ndege wa Port
Said.
Baada
ya tukio hilo idadi maalum iliwekwa kwa watakaohudhuria Mechi kwa hofu ya hali
ya usalama ,inaelezwa kuwa mipaka hiyo iliyoondolewa hivi karibuni huwenda
ikawekwa tena baada ya tukio la mwishoni mwa juma lililopita.
Chanzo: BBC Swahili.
Post a Comment