Huyu ndiye kiongozi wa upinzani nchini Malaysia, Anwar Ibrahimu, anakabiliwa na kifungo akipatikana na hatia.
Hatima ya kiongozi wa upinzani nchini Malaysia Anwar Ibrahim ni mwezi march mwaka huu iwapo atafungwa jela ama kuwa huru dhidi ya mashtaka yake ya ulawiti.


Mahakama kuu ya Malaysia inatarajiwa kupitia rufani ya Anwar aliyekutwa  na makosa ya kufanya mapenzi ya jinsia moja na msaidizi wake wa kiume mwaka 2008.

Hata hivyo Anwar mwenyewe anasema kuwa mashtaka haya dhidi yake ni sehemu ya kampeni za kisiasa kutaka kumpunguzia hadi yake zinazofanywa na chama tawala cha UMNO.

Anwar aliyekuwa naibu waziri mkuu wa Malaysia miaka ya 90 alijiunga na upinzani, na alifungwa jela kwa miaka sita baada ya kubainika na makosa ya ufisadi na mapenzi ya jinsia moja kabla ya mashtaka mengine kama hayo yaliyomkumba kwa mara ya pili.

Chanzo:  BBC News!

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Asante kwa kutembelea mtandao huu

Post a Comment

 
Top