Watu wa familia moja waliouawa huko Caroline Kazkazini

Maafisa wa polisi mjini Carolina kaskazini nchini Marekani wamemkamata mtu mmoja baada ya wanafunzi watatu waislamu kukutwa wamefariki nyumbani mwao.

Miili ya Deah Barakat, mkewe Yusor Mohammed Abu salha na dadaake Razan Mohammed Abu salha ilipatikana siku ya Jumanne ikiwa na majeraha ya risasi katika vichwa .

Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 46 tayari amefunguliwa mashtaka kutokana na mauaji hayo.

Maafisa wa polisi wanasema wanajaribu kubaini iwapo mauaji hayo yanatokana na chuki.

Swala kwamba wanafunzi waliouawa ni waislamu limezua uvumi katika mitandao ya kijamii wa iwapo mauaji hayo ni ya kidini au la.

Uchunguzi uliofanywa umebaini kwamba uhalifu huo ulitekelezwa kutokana na mzozo unaondelea kuhusu uegeshaji wa magari,maafisa wa polisi wa Chapell wamesema.

Source: Kwa hisani ya BBC Swahili News
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Asante kwa kutembelea mtandao huu

Post a Comment

 
Top