Kwa asiye mkazi wa Shinyanga, hapa ni katikati ya mji wa Shinyanga, barabara kuu ya Nkurumah kushoto lipo jengo la ghorofa mbili ambapo ndani yake kuna benki ya Posta.
Hizi ni baadhi ya barabara zinazotarajiwa kufungwa kwa lengo la kubadili matumizi yake ili sasa zipimwe viwanja vya makazi.
MAKUBWA HAYA!!! PAMOJA NA SHINYANGA KUWA NI MIKOA YENYE RASLIMALI NYINGI ZA ASILI IKIWEMO MADINI YA ALMASI NA DHAHABU, LAKINI BADO MAKAO MAKUU YA MJI HUO HAYANA TOFAUTI NA MIKOA AMBAYO HAINA RASLIMALI HIZO.


HALI HIYO INADHIHIRISHWA NA JINSI MIUNDOMBINU YAKE YA  BARABARA KWA MBOVU KATIKA MAENEO YOTE YA MJI HUO HATA ZILE ZILIZOJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI KIWANGO CHAKE NI CHA CHINI SANA..

ANGALIA MWENYEWE HII NI MOJA YA BARABARA ILIYOPO KATI KATI YA MJI WA SHINYANGA, ENEO LA BENKI YA POSTA, MADIMBWI YA MAJI YAMEFURIKA KIASI CHA KUSABABISHA MAGARI NA WATEMBEA KWA MIGUU KUTEMBEA KWA SHIDA!

WAKAZI WA MJI HUO WAMEKUWA WAKIHOJI NI VIPI WATENDAJI WA MANISPAA PAMOJA NA WAWAKILISHI WAO, MADIWANI WAMESHINDWA KUIONA ADHA HIYO AMBAPO WAMESHINDWA HATA KUFUKIA KWA VIFUSI MADIMBWI YA MAJI YALIYOFURIKA KUTOKANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA MASIKA KAMILI.

HATA HIVYO WAKATI MANISPAA IKISHINDWA KUZIFANYIA UKARABATI BARABARA ZAKE, HIVI KARIBUNI MADIWANI WA MJI HUO KUPITIA VIKAO VYAO MBALIMBALI IKIWEMO BARAZA LA MADIWANI WALIBARIKI KUFUNGWA KWA BAADHI YA BARABARA ZILIZOPO KATIKATI YA MJI HUO NA BADALA YAKE ZIPIMWE VIWANJA VYA MAKAZI, KITENDO AMBACHO WANANCHI WENGI WAMEKIONA KUWA NI MOJA YA VITUKO VYA MWAKA IWAPO BARABARA HIZO ZITAFUNGWA NA BADALA YAKE KUJENGWA NYUMBA ZA MAKAZI.

JE!!! WANANCHI WA SHINYANGA TUFANYEJE KUEPUKANA NA ADHA HII BAADA YA WAWAKILISHI WETU KUONEKANA WAMEVAA MIWANI YA MBAO KIASI YA KUTOKULIIONA TATIZO???? -  TUJADILI!!!
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Asante kwa kutembelea mtandao huu

Post a Comment

 
Top