ISOME HUKUMU YA WANAOENDELEZA TABIA KUHARIBU SEHEMU ZA SIRI ZA WATOTO WA KIKE, ETI UKEKETAJI!!!


Katika kesi ya kipekee nchini Misri, daktari mmoja ametiwa mbaroni kwa kosa la kumkeketa msichana mwenye umri wa miaka kumi na tatu.

Awali wakereketwa wanaopinga tabia ya kuwakeketa watoto wa kike, walishtuka baada ya mahakama ya nchini humo kumwachilia huru Daktari Raslan Fadl mwezi Novemba mwaka jana.

Lakini baada ya kesi kusikizwa upya, amehukumiwa zaidi ya miaka miwili gerezani.

Ingawa ukeketaji wa wasichana ulipigwa marufuku miaka sita iliyopita nchini Misri, zoezi hilo bado linaenea pakubwa.

Wale ambao wanajaribu kupambana na ukatili huo wameelezea hukumu ya Daktari Fadl kuwa ni ushindi mkubwa kwao.

Source: BBC News.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Asante kwa kutembelea mtandao huu

Post a Comment

 
Top