|
Safu ya viongozi wa Kitaifa, kuanzia kushoto ni Katibu Mkuu wa CHODAWU Taifa, Said S. Wamba, Mwenyekiti wa Taifa, Wilfred Mshana, Mwenyekiti wa Taifa kamati ya wanawake CHODAWU, Agnes Barabojick na Naibu Katibu Mkuu, Abraham Muhoja. |
|
Wajumbe wa kamati ya Utendaji Taifa CHODAWU wakiwa katika picha ya pamoja |
|
Wajumbe wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima kabla ya kikao chao. |
|
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji CHODAWU Taifa wakiendelea na kikao chao jijini Dar es Salaam |
CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA HIFADHI, MAHOTEL, MAJUMBANI, HUDUMA ZA JAMII NA
USHAURI (CHODAWU) KIMETANGAZA DHAMIRA YAKE YA KUPAMBANA NA WAAJIRI
WAKOROFI WASIO WATENDEA HAKI WAFANYAKAZI WAO WA NDANI, IKIWEMO KUWAPA
LIKIZO, KUWAPUNJA MISHAHARA NA KUWANYANYASA HUKU WAKIWAFANYISHA KAZI KWA
MASAA MENGI BILA KUWAPATIA MUDA WA KUPUMZIKA.
AZIMIO HILO LIMEFIKIWA KATIKA KIKAO CHA KAMATI YA UTENDAJI CHODAWU TAIFA
KILICHOFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM AMBAPO PIA SUALA LA UFUNGAJI WA
MIKATABA YA HALI BORA YA KAZI LIMESISITIZWA NA KUTOA WITO KWA
WAFANYAKAZI KUSHINIKIZA WAAJIRI KUPITIA MATAWI YAO YA CHODAWU
KUHAKIKISHA MIKATABA HIYO INAFUNGWA KATIKA MAENEO YOTE YANAYOTIMIZA
MASHARTI YA UFUNGWAJI WAKE.
Post a Comment