CHAMA
Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewataka viongozi wa serikali ya CCM
kuacha kutumia vibaya madaraka waliyonayo huku wakiwagawa watanzania kwa misingi
ya kimatabaka mambo yaliyopigwa vita na hayati baba wa Taifa, Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere. Akihutubia
maelfu ya wakazi wa mji wa Shinyanga na vitongoji vyake katika mkutano wa
hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya mahakama ya mwanzo mjini humo,
mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa vijana wa CHADEMA (BAVICHA), Paschal Katambi
alisema serikali ya CCM imeanza dalili za kuonesha kutoheshimu haki na misingi ya
kibinadamu.
Katambi
alisema
wapo viongozi wengi ndani ya serikali wamekuwa wakitumia vibaya
madaraka yao kwa misingi ya kukiwezesha Chama cha Mapinduzi kiendelee
kutawala daima katika nchi hii ambapo kwa wale wanaoonesha kutokiunga
mkono chama hicho wamekuwa wakipata matatizo ikiwemo kukamatwa na polisi
wengine kukumbwa na vifo vya mashaka.
Alisema
katika maeneo mengi hivi sasa wananchi wanaolalamika
kutotendewa haki na watendaji wa serikali wakinyimwa haki zao za msingi
na kutendewa vitendo vinavyopingana na haki za kibinadamu hali ambayo
imechangia malalamiko
mengi mfano wa migogoro ya ardhi iliyoshamiri sehemu nyingi nchini.
Mbali
ya
migogoro ya ardhi ambapo wananchi kila kunapokucha wanafukuzwa kutoka
katika maeneo
yao ili kuwapisha wawekezaji wa kigeni lakini pia lipo tatizo la
viongozi wa CCM kulitumia vibaya Jeshi la Polisi ili kulinda maslahi ya
chama chao kwa lengo kukiwezesha kiendelee kutawala
daima japokuwa wananchi wamekichoka.
Post a Comment