Wajumbe wa kikao cha Baraza Kuu la Jumuiya ya UWT wilaya ya Shinyanga vijijini wakifuatilia kwa makini kikao. |
Mbunge Azza Hillal akizungumza na baadhi ya wajumbe wa Jumuiya ya UWT wilaya ya Shinyanga vijijini baada ya kukabidhi baiskeli 20 za walemavu. |
Mbunge wa viti maalumu akimpongeza mmoja wa walemavu baada ya kumkabidhi baiskeli ya walemavu, ambapo mlemavu huyo alishukuru kwa kueleza baiskeli hiyo itamsaidia sana katika shughuli zake. |
Mbunge wa viti maalum Azza Hillal akimpongeza mmoja wa walemavu kutoka Shinyanga vijijini muda mfupi baada ya kumkabidhi kiti cha kumsaidia kutembea. |
Tahadhari hiyo imetolewa na mbunge wa viti maalumu mkoani Shinyanga, Azza Hillal alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Baraza la Jumuiya ya UWT wilaya ya Shinyanga vijijini ambapo aliwataka wawe makini na kujiepusha na ushabiki wa aina yoyote unaoweza kusababisha nchi kuingia katika machafuko katika kipindi hiki cha mjadala wa rasimu ya katiba mpya.
Azza alisema iwapo Tanzania itaingia katika vurugu watu wa kwanza watakaoathirika kwa kiasi kikubwa ni wanawake na watoto ambao hukumbuna na majanga ya ubakwaji na kulawitiwa na kwamba ni jukumu lao kuhakikisha hali ya amani na utulivu uliopo hivi sasa nchini haitoweki na hakuna mtu anayeichezea.
Alisema mataifa mengi ulimwenguni ambayo yaliyojaribu kubadili katiba zao yalijikuta yakiingia katika vurugu kubwa kiasi cha kusababisha kutokea kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe hali ambayo haipaswi kutokea kwa Tanzania ambayo wananchi wake kwa kipindi kirefu wamelelewa na kukulia katika hali ya amani na utulivu chini ya serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
“Mchakato wa mabadiliko ya katiba ni siasa, tusidanganyane, wakati wa zoezi hili kila chama hujitahidi na kuhakikisha masuala muhimu yenye maslahi kwake yanaingia ndani ya katiba, sasa mvutano unaondelea hivi sasa hapa kwetu siyo jambo la ajabu, CCM lazima tusimame kidete tupiganie maoni yetu yaweza kupata nafasi ndani ya katiba mpya,”
“Ndugu zangu lazima hapa tuelezane ukweli, hawa wanaoshabikia muundo wa serikali tatu hawana nia njema na nchi yetu hasa upande wa suala la muungano, muundo wa kila nchi kuwa na serikali yake na kisha kuwepo serikali ya shirikisho utaathari kwa kiasi kubwa muundo wa muungano wetu, tuwe makini,”
“Lakini eleweni wanaoshabikia muundo wa serikali tatu wana uhakika kabisa iwapo nchi itaingia katika vurugu watakimbilia nje ya nchi na familia zao, niwaulize ninyi mama zangu na dada zangu msiokuwa na jamaa nje, mtakimbilia wapi?, hivyo tuwe makini na mabadiliko ya katiba, tuwaelimishane kwamba muundo sahihi ni serikali mbili,” alisema.
Kwa upande mwingine mbunge huyo aliwataka akinamama wote ndani ya CCM kupitia jumuiya yao ya UWT kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya kushiriki katika chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2015.
“Kipindi cha chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2015 hivi sasa kimekaribia, ni muhimu sasa tukajiandaa mapema kwa kujipanga vizuri ili kukiwezesha chama chetu kiweze kuibuka na ushindi wa kishindo katika nafasi zote ikiwemo kukamata dola, lazima CCM iendelee kutawala,” alieleza Azza.
Post a Comment