Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Justin Sheka (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya madiwani wake wakiangalia moja ya miradi inayotekelezwa wilayani Kishapu. |
Miradi mikubwa kama hii inaweza kukwama iwapo halmashauri haitopata vyanzo vya kutosha vya fedha ambazo karibu nusu ya mapato yake ya ndani hutokana na ushuru wa zao la pamba. |
Sehemu ya majengo ya hospitali mpya ya wilaya ya Kishapu ambayo iko katika hatua za mwisho za kukamilika ujenzi wake. |
Wakitoa taarifa rasmi ya kusudio hilo kwa waandishi wa habari mjini Mhunze muda mfupi baada ya kikao chao cha baraza la madiwani walisema hawakubaliani na agizo la waziri mkuu kwa vile wasipokusanya ushuru huo kutaathiri kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika halmashauri yao.
Walisema kwa kipindi kirefu halmashauri yao imekuwa ikitekeleza miradi ya maendeleo kwa kutumia mapato ya ndani ambayo nusu yake hukusanywa kutoka katika ushuru wa zao la pamba na kwamba agizo la waziri mkuu kuiagiza Bodi ya pamba kukusanya ushuru huo ni kutaka kukwamisha miradi hiyo.
Akifafanua kuhusu kusudio hilo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Justin Sheka alisema iwapo waziri mkuu hatatengua agizo lake madiwani watatembea kila kijiji kuwahamasisha wakulima waache kulima pamba na sasa walime mazao mbadala ya biashara ili waone iwapo bodi ya pamba itaendelea kuwepo nchini.
“Tumesikitishwa sana na agizo la waziri mkuu, tunashangaa ametoa agizo hilo bila hata bila ya kutushirikisha, Bodi ya pamba kwa kipindi kirefu imeshindwa kumsaida mkulima hata kwa kumtafutia soko zuri lenye bei kubwa au hata kumuwezesha aweze kulima kitaalamu badala yake waziri mkuu anawaongezea jukumu lingine,”
“Hili agizo sisi litatuathiri sana, nafikiri waziri mkuu alishauriwa vibaya, tunaendelea kumuomba apitie upya agizo lake, maana iwapo wakulima watahamasishwa na waachane na kilimo cha pamba hata serikali kwa upande wake itaathirika kwa kiasi kikubwa na pia baadhi ya viwanda vya nguo vitakosa malighafi,” alieleza Sheka.
Sheka alisema ushuru wa zao la pamba ulikuwa ni mhimili muhimu katika halmashauri yake kwa vile sehemu ya fedha hutolewa kwa maofisa ugani ili kuwawezesha kwenda vijijini ambako huwasaidia wakulima zao hilo waweze kulima pamba yao kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo kazi ambayo ilipaswa kutekelezwa na bodi ya pamba.
“Wakulima wetu wanaweza kulima mazao mengine ya kibiashara kama vile choroko, alizeti, mpunga na dengu ambayo katika siku za hivi karibuni yameonesha kuwa na bei nzuri kuliko pamba na hivyo kujianzishia bodi nyingine hata kama itaitwa Bodi ya Alizeti, na waachane na bodi ya pamba,” alieleza Sheka.
Naye diwani wa kata ya Mwadui Lohumbo Paulo Magembe (CHADEMA), alisema agizo la waziri mkuu mbali ya kuathiri utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyopangwa kutekelezwa na halmashauri hiyo litachangia pia kukwamisha utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ikiwemo suala la kuwapatia watanzania maisha bora.
Magembe alisema serikali ya CCM inapaswa kuhakikisha inawatekelezea wananchi wake kile ilichowaahidi mwaka 2010 vinginevyo watakuwa na kila sababu ya kuangalia chama mbadala ambacho watakikabidhi jukumu la kuunda serikali na kwamba agizo la waziri mkuu limetolewa kibabe zaidi kwa vile hapakuwa na ushirikishwaji.
“Agizo la waziri mkuu kuitaka Bodi ya pamba ikusanye ushuru huu linaondoa ile dhana ya kuanzishwa kwa serikali za mtaa ambayo ni kusogeza huduma kwa wananchi inapotea, maana serikali kuu sasa imechukua mapato yote na kudai tutarejeshewa siyo kweli, maana hata ile ruzuku ya kisheria sasa hivi hailetwi,” alieleza.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.