Mkurugenzi wa Asela Promotion ya Mjini Kahama mkoa wa Shinyanga, Asela Magaka akikabidhi kwa mmoja wa walimu wa shule ya msingi Buhangija Jumuishi, mwalimu Bright Mduma msaada kwa ajili ya kuwasaidia watoto walemavu wa ngozi (Albinism) wanaotunzwa katika kituo hicho.

WAREMBO 20 WANAOWANIA TAJI LA MISS TALENT SHINYANGA NA MISS SHINYANGA 2014 LEO WAMEWATEMBELEA WATOTO WALEMAVU WA NGOZI (ALBINISM) WANAOTUNZWA KATIKA KITUO CHA SHULE YA MSINGI BUHANGIJA JUMUISHI MANISPAA YA SHINYANGA WAKIONGOZWA NA MRATIBU WA MASHINDANO HAYO, ASELA MAGAKA WA ASELA PROMOTION.


KATIKA ZIARA HIYO ASELA MAGAKA KWA NIABA YA KAMPUNI YAKE YA ASELA PROMOTION ALITOA MSAADA WA VYAKULA MBALIMBALI IKIWEMO, SABUNI ZA KUFULIA NA CHUMVI VYOTE VIKIWA NA THAMANI YA SHILINGI 506,700 AMBAPO PIA ALICHANGIA MIFUKO MITANO YA SARUJI KWA AJILI YA KUSAIDIA UJENZI WA BWENI LINALOJENGWA NA ALIYEKUWA MISS TANZANIA 20O3/20O4, BRIGTA ALFRED.

KWA UPANDE WAO WANYANGE WANAOWANIA TAJI HILO LA MISS TALENT SHINYANGA NA MISS SHINYANGA 2014 NA WAKUFUNZI WAO PIA WALICHANGIA MIFUKO YA SARUJI, NGANO NA FEDHA TASLIMU SHILINGI 200,000 KWA AJILI YA KUSAIDIA UJENZI WA BWENI HILO LINALOJENGWA NA MISS TANZANIA 2003/2004. MISAADA YOTE ILIYOTOLEWA ILIKUWA NA THAMANI YA SHILINGI 996,700.

ANGALIA PICHA ZA WAREMBO HAO:

Mkurugenzi wa Asela Promotion ya Mjini Kahama mkoa wa Shinyanga, Asela Magaka akikabidhi kwa mmoja wa walimu wa shule ya msingi Buhangija Jumuishi, mwalimu Bright Mduma msaada kwa ajili ya kuwasaidia watoto walemavu wa ngozi (Albinism) wanaotunzwa katika kituo hicho.


Baadhi ya warembo wakiwa pamoja na watoto wenye ulemavu wa ngozi (albinism) muda mfupi kabla ya kukabidhi misaada waliyokuwa nayo.
Mmoja wa warembo hao Neema Kakimpa kutoka wilaya ya Kahama akikabidhi kwa mwalimu Bright Mduma msaada wake wa fedha taslimu kiasi cha shilingi 40,000 kwa ajili ya kununulia mifuko miwili ya saruji
Wakufunzi wa warembo wanaowania Taji la Miss Shinyanga Talent na Miss Shinyanga 2014 wakiwa wamepozi na mmoja wa watoto wenye ulemavu wa ngozi albinism.

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Asante kwa kutembelea mtandao huu

Post a Comment

 
Top