Ofisa kutoka PINGOs Forum, Emmanuel Saringe akizungumza na wafugaji wa kijiji cha Ihushi wilayani Bariadi mkoa wa Simiyu.
SIMIYU
BAADHI ya wafugaji katika wilaya za Meatu na Bariadi mkoani Simiyu wamelalamikia kitendo cha kukamatwa ovyo na askari wanyamapori kwa madai ya kuingiza ng’ombe zao ndani ya maeneo ya hifadhi ambapo hutozwa faini kubwa kinyume cha sheria na kutopewa stakabadhi zozote.
Hata hivyo wafugaji hao wamedai maeneo mengi yanayodaiwa kuwa ni sehemu ya hifadhi yalichukuliwa bila ya wao kushirikishwa huku wakitoa mfano wa udanganyifu uliofanyika kwa wakazi wa vijijij saba wilayani Meatu walioshawishiwa kuanzisha eneo la hifadhi ya jamii (WMA).

Wakifafanua hivi karibuni mbele ya maofisa wa Shirika la PINGO’s Forum wafugaji hao walidai mara kwa mara wanapokamatwa na askari wanyamapori hutozwa faini kati ya shilingi 500,000 hadi milioni 10 kulingana na idadi ya ng’ombe waliokamatwa ambapo hata hivyo walidai wanapolipa fedha hizo hakuna stakabadhi zozote wanazopewa.
Walisema hivi sasa wafugaji wanaoishi kandokando ya maeneo ya hifadhi ya Maswa Game reserve katika wilaya za Bariadi na Meata na pori la hifadhi ya jamii ya Makao wilayani Meatu wamegeuka kuwa vitega uchumi wa askari wanyamapori hali ambayo isipodhibitiwa mapema inaweza kusababisha kutokea mapigano.
Mmoja wa wafugaji hao, Mlanduda Gwaigeshi alidai yeye binafsi ng’ombe wake waliwahi kukamatwa kandokando ya hifadhi ya Makao (WMA) na kutakiwa alipe faini ya shilingi milioni 10 hata hivyo alipolalamika alilipishwa shilingi milioni tano na hakupewa stakabadhi yoyote.
Kwa upande wake Jilalabo Bida alilalamikia kitendo cha serikali kuwageuka wakazi wa vijiji vya Mbushi, Makao, Jinamo, Sapa, Mwabagimu, Irambandogo na Mwagundo vinavyounda hifadhi ya ya Jamii (WMA) ambapo wakati wa uundwaji wa hifadhi hiyo walithibitishiwa itakapoanzishwa watakuwa wakiruhusiwa kuchungia mifugo yao hata hivyo ilipoanza walikatazwa.
“Wakati sisi wakazi wa vijiji hivi sasa tukiombwa kutoa maeneo ya ardhi yetu kwa ajili ya uundwaji wa hifadhi ya kijamii tulielezwa wazi kwamba kipindi cha kiangazi tutaruhusiwa kuingiza ng’ombe wetu kwa ajili ya kutafuta malisho, lakini mambo yamekuwa kinyume chake, hata tunapoomba kujitoa haturuhusiwi,” alieleza Bida.
Wafugaji hao wameiomba serikali isikilize kilio chao cha ukosefu wa maeneo ya malisho ambapo wameshauri kutengewa maeneo rasmi watakayoendeshea shughuli zao za ufugaji kama inavyofanyika kwa wanyamapori wanaotengewa maeneo ya hifadhi na kwamba ufugaji wa kisasa hautokuwa na tija iwapo wafugaji hawatatengewa maeneo ya malisho.
Akifafanua kuhusiana na suala la utozwaji wa faini pasipo kutoa stakabadhi kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Meatu, Ofisa wanyamapori wilayani Meatu Mohamed Omari alisema kitendo kinachofanywa na askari wanyamapori ni kinyume cha utaratibu na kuahidi kulifanyia kazi tatizo hilo.
Mwisho.
Post a Comment