MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cham mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Kikwete amesema serikali itamalizia ujenzi wa hospitali ya rufaa ya Kwangwa iliyopo mijini Musoma kwa ajili ya kusogeza huduma bora za afya kwa wananchi wengi wengi katika mkoa wa Mara na mikoa ya jirani.

Rais Kikwete alitoa ahadi hiyo juzi mjini Musoma alipokuwa akiuhutibia umati wa watu waliokusanyika kusikiliza mkutano wa kampeni za CCM ambapo alisema hospitali hiyo imekaa kwa muda mrefu baada ya kanisa katoliki kushindwa kuiendeleza lakini serikali inaubeba mzigo huo.

“Hii hospitali ni muhimu sana kwa kutoa hudduma hususan kwa nanchi wengi wa mara na mikoa ya jirani ambao hulazimika kusafiri hadi mwanza na maeneo mengine kwa ajili ya kupata huduma ya rufani, lakini sasa tutaijenga na kuikamilisha ili itoe huduma.

Kwa mujibu wa Rais Kikwete tayari suala hilo limeshawekewa misingi imara na pindi CCM itakapochaguliwa kuuongoza nchi katika kipindi cha miaka mitano ijayo, hospitali hiyo itaweza kutoa huduma kama ilivyokusudiwa.

Awali hospitali hiyo ilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi kabla ya kanisa katoliki kuiomba ambapo hata hivyo ilishindwa kuimalizia na kuiomba serikali kuendelea na taratibu za kuhakikisha inakamilika na kuwahudumia wananchi.

Mbali na kuahidi ujenzi wa hospitali hiyo, Rais Kikwete pia aliwaahidi wana-Musoma waliovunja rekodi kwa mahudurio katika mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Mukendo, kuwa seriakali ya CCM pia itaongeza kazi katika ujenzi na uboreshaji wa sekta ya miundombinu ili kuwa na mawasiliano mazuri baina ya mkoa huo na mikoa mingine.

Alisema tayari mpango wa ujenzi wa barabara kubwa itakayounganisha Musoma kupitia mugumu, Serengeti, Ngorongoro hadi Mto wa Mbu ipo katika hatua nzuri na kikwazo kilichosalia ni maneno maneno yatokayo kwa baadhi ya watu kuhusu kuipitisha barabara hiyo katika mbuga ya wanyama ya Serernge.

Hata hivyo alisema licha ya kuithamini mbuga hiyo lakini wananchi wa Loliondo, na mamengine yaliyokaribu na mbuga hiyo wana haki ya kupata huduma bora za kijamii ikiwemo barabara.

“Hivi ni kweli tukubali kuwaacha wananchi wakose huduma muhimu kwa kikwazo hiki ambapo hata hivyo hatujasema kuwa tutaathiri mbuga hiyo, ni maneno maneno tu ya baadhi ya watu ambayo hata hivyo hayakufanyiwa utafiti wa kutosha.

Awali akizungumza katika mkutano huo mbunge wa jimbo hilo Vedastus Mathayo alisema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita CCM imetekleleza kwa vitendo Ilani yake ya mwaka 2005.

Hata hivyo aliwao,mba wananchi kuipa nafasi CCM katika kipindi kingine ili iweze kuendeleza miradi yake ya maendeleo iliyoianza miaka mitano iliyopita.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Asante kwa kutembelea mtandao huu

Post a Comment

 
Top