Papa Francis ameagiza marufuku ya uuzaji wa
sigara ndani ya Vatican , kuanzia mwaka ujao.
Msemaji wa Vatican Greg Burke alisema kuwa mji
huo mtakatifu hauwezi kukubali na kitendo ambacho kinahatarisha maisha ya
binaadamu.
Takriban wafanyikazi 5000 wa Vatican na wale
waliostaafu wanaruhusiwa kununua sigara zilizopunguzwa bei.
Mauzo hayo yanakadiriwa kuiletea Vatican
mamilioni ya yuro kila mwaka.
Lakini bwana Burke amesema kuwa hakuna faida
ambayo ni halali iwapo sigara zinaathiri afya za wanaadamu.
Alinukuu takwimu za shirika la afya duniani WHO
ambazo zinalaumu uvutaji sigara kwa kusababisha vifo vya takriban watu miioni 7
duniani kila mwaka.
''Nadhani watu wengi wanapenda sigara kwa
sababu ya ufadhili wanaopata'' ,alisema.
''Ni kitu ambacho ni lazima kufutilia mbali
licha ya kuleta mapato Vatican, muhimu ni kufanya kile kilicho sawa''.
Papa Francis ambaye pafu lake moja liliondolewa
wakati alipokuwa kijana havuti sigara.
Wafanyikazi wa vatican na wale waliostaafu
wanaruhusiwa kununua pakiti tano za sigara kila mwezi kutoka kwa duka
lisilotozwa ushuru.
Source: BBC Swahili News.
Post a Comment