KADA ANAYEANZA KUCHIPUKIA NDANI YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA), KHAMIS MGEJA, AMEKIONYA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) KISIJARIBU KUTUMIA STAILI YA KUFUNGA "GOLI LA MKONO" KATIKA UCHAGUZI MDOGO UJAO WA MADIWANI UTAKAOFANYIKA KATIKA KATA 20 NA UBUNGE KATIKA JIMBO LA DIMANI KULE ZANZIBAR MNAMO JANUARI 22, MWAKA HUU.

MWANAHABARI HASTIN LIUMBA ANARIPOTI KUTOKA KULE MULEBA MKOANI KAGERA:


KADA machachari wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Khamis
Mgeja ameionya chama cha mapinduzi (CCM) kiache mchezo mchafu wa ‘Goli
la Mkono’ ambao ni sawa na wizi wa kura katika chaguzi ndogo za
Udiwani na Ubunge zinazofanyika nchini sasa.

Mgeja aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika
katika kijiji cha Kiota kata ya Kimwani wilaya ya Muleba mkoa wa
Kagera wakati akimnadi mgombea udiwani kwa tiketi ya Chadema Lenard
Nchimwani.

Kada huyo alisema wanazo taarifa kuwa CCM baada ya kuona
wameshaelemewa na wananchi wameshawachoka maeneo mengi nchini na
dalili ya kushindwa iko wazi hivi sasa wameamua kujipanga kwa ‘Goli la
Mkono’ ambao tunaona ni wizi wa kura.

“Ila mkakati wao wanaona,wanadhani utawaokoa kupita kila nyumba kugawa
chumvi, Khanga, fulana, kofia na sh 5,000 lakini pia imebakiza
rasilimali za kubebwa lakini hawabebeki …..tunaiomba TAKUKURU
ifuatilie ‘Tuhuma’ hizi kama kweli zina ukweli ndani yake hasa siku ya
usiku wa kuamkia kupiga kura.”alisema.

Alisema lakini tumejiandaa udhalimu wa mchezo mchafu wa goli la mkono
kwani kauli hii ambayo iliwahi kutolewa na aliyekuwa katibu wa itikadi
na uenezi  taifa Nape Nnauye mwaka wa uchaguzi uliopita wa  2015, na
sasa kuelekea katika chaguzi ndogo ,katika chaguzi za serikali za
mitaa 2019 na uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.

Mgeja alitahadharisha wapiga kura wanaounga mkono mabadiliko kuwa
macho na kutokubali kununuliwa kwa ‘kitu kidogo’ na hatimaye kuuza
haki yao ya kupiga kura na hatimaye kuwagharimu kwa kipindi cha miaka
mitano ijayo.

Alisema CCM sasa hivi haina Pumzi imebaki kuweweseka na ile CCM ya
Hayati Mwalimu Julias Kambarage Nyerere sasa hivi haipo..CCM
ninayoifahamu mimi siyo hii iliyopo sasa imebaki jina tu la Bendera.

“Leo watanzania mmeona tulipofika,pia mnaona mwenyekiti wa CCM taifa
Dk John Pombe Magufuli anavyotumbua majipu kila wizara sasa lazima
tujiulize je! haya majipu nani kayafuga na kuyalea?…..wananchi
walipiga kelele kwa kujibu CC eeeeeeeeeeee M.”alisema.

Alisema hapa tulipofikia nchi kupinda ni chama cha mapinduzi (CCM)
lazima ibebe lawama kwani wao ndio waliokabidhiwa kuongoza nchi wala
siyo mtu.

Alisema ukiona wizi unatamalaki nchini,ufisadi,mishahara
hewa,makontena hewa,wanafunzi hewa na maeneo mengi ni uchafu ikiwemo
mikataba mibovu ya madini, mwenyekiti wa CCM Dk John Magufuli
alikuwemo  na kwenye kikao muhimu cha baraza la mawaziri kwa kipindi
cha miaka 20 yote haya hakuyaona.

Alisema hapa hawezi kukwepa lawama kwani naye alikuwemo kwenye hiyo
nyumba ya CCM wakati uchafu huo unafanyika.

Mgeja alisema CCM wangekuwa waungwana ingewaomba radhi wananchi hapa
ilipowafikisha ukiwemo umasikini mkubwa wa kutisha na rushwa
iliyotamalaki na huko ndiko kuishiwa Punzi.

“Namuomba Katibu mkuu wa CCM taifa Abdulrahaman Kinana kwa niaba ya
chama chake ajitokeze hadharani kwa niaba ya chama chake awaombe radhi
wananchi kwa hapa CCM ilipotufikisha.

Kada huyo alisema watanzania wana kiu na hari ya mabadiliko kwa safari
ya mabadiliko tayari tumeshafika na duniani sasa hivi wananchi
wanataka mabadiliko kama vile nchi za Marekani,Gambia,Ghana na
kwingineko wamefanya mabadiliko na mabadiliko kwa Tanzania ya sasa
inawezekana.

Aidha Mgeja aliwaomba watanzania wajitambue,watambue haki zao za
huduma za jamii kuwa ni wajibu wa serikali wala huduma hizo za jamii
siyo hisani kutoka serikalini.

Mgeja aliwaomba wananchi wa kata ya Kimwani wamchague mgembea wa
udiwani kupitia Chadema ili salamu ziwafikie CCM kuwa watanzania
wamewachoka na wanataka mabadiliko.

Katika kampeni hizo ilihudhuriwa na mjumbe wa kamati kuu ya Chadema
taifa Edward Lowassa,mbunge wa Chadema Wilfred Lwakatare,mstahiki Meya
wa Bukoba  Chifu Kalumuna,mkurugenzi wa fedha taifa wa Chadema Lodrick
Lutembeka na viongozi wengineo wa chama hicho.


Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Asante kwa kutembelea mtandao huu

Post a Comment

 
Top