Rais mstaafu wa awamu ya nne na mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto) akiteta jambo na rais wa awamu ya tano, Dkt. John Magufuli katika moja ya vikao vya CCM, kulia ni katibu mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana.
RAIS Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete bado ataendelea kuwa kiongozi mkuu hapa nchini baada ya kushindikana kufanyika kwa mkutano mkuu wa chama chake cha Mapinduzi (CCM) ili amkabidhi rais aliyepo madarakani hivi sasa, Dkt. John Pombe Magufuli.


Hali hiyo inatokana na kushindikana kufanyika kwa mkutano mkuu wa CCM Taifa ambao agenda yake kuu ilikuwa ni kumkabidhi rasmi Dkt. Magufuli mikoba ya UENYEKITI wa Taifa wa CCM.

Kwa hali hiyo, na kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni wazi kuwa kiongozi mkuu katika nchi hii bado ataendelea kuwa Kikwete kwa vile katiba ya mwaka 1977 toleo la 2005 inaeleza wazi kuwa Chama kitakachoshinda katika uchaguzi mkuu ndicho kitakachokabidhiwa jukumu la kuunda serikali.

Habari zaidi ipate hapa:

Link: http://www.ippmedia.com/sw/habari/mkutano-mkuu-maalum-wa-ccm-waota-mbawa?utm_campaign=shareaholic&utm_medium=email_this&utm_source=email -
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Asante kwa kutembelea mtandao huu

Post a Comment

 
Top