Wachezaji wa timu ya Chile wakishangilia wakiwa na kombe lao la ubingwa wa michuano maalumu ya Copa America. |
Argentina
imehitimisha miaka 23 bila kupata kombe lolote na Messi alikuwa na nafasi kubwa
ya kushinda angalau mara moja hasa katika michuano ijayo ya kombe la dunia
itakayofanyika mwaka 2018 nichini Urusi akiwa na miaka 31 lakini hilo
halitafikiwa tena hii ni baada ya mshambuliaji huyo kuamua kustaafu kuichezea
timu hiyo.
Argentina
wamepoteza fainali tatu mfululizo ndani ya miaka mitatu hii wakianza na fainali
a kombe la dinia mwaka 2014 wakicheza na Ujerumani, mwaka jana 2015 walifungwa
katika fainali ya kombe la Copa America dhidi ya Chile, inauma sana Messi
alisikika akiwambia wenzake wakati akiwaagaa rasmi na kuachana na soka la
kimataifa kwa ngazi ya timu za taifa.
Chile,
ambayo ilisubiri kwa takribani miaka 99 ili kushinda kombe la Copa America,
walifanikiwa kutwaa taji hilo nyumbani kwao katika mji wa Santiago na sasa tena
wamefanya hivyo nchini Marekani katika mji wa New Jersey, lakini safari hii
ikiwa ni michuano maalumu ya maadhimisho ya miaka 100 ya michuano ya Copa
America, ni rekodi ya aina yake kwa kizazi kipya cha dhahabu cha Chile na
wamefanikiwa.
Mchezaji maarufu wa Kambumbu Leone Messi (10) alichangia Taifa lake kukosa ubingwa wa kombe la Copa Amerika baada ya kupaisha juu mkwaju wake wa penati. |
Mchezo huo
wa fainali iliyotawaliwa na mchezo wa ufundi na nguvu nyingi na rafu za hapa na
pale ulidumu kwa dakika Dakika 120 baada ya awali kushuhudia timu hizo kucheza
dakika 90 bila kuona mlango wa mwingine na hali hiyo ilikuwa hata katika dakika
30 za nyongeza za muda wa ziada wa mchezo huo ambazo nazo zilishuhudia timu
hizo zikienda suluhu ya bila kufungana.
Katika
mchezo huo ambao kwa kiasi kikubwa ulitawaliwa na ubabe wa hapa na pale huku
ikushuhudiwa timu zote mbili zikimaliza kipindi cha kwanza zikiwa na wachezaji
10 baada ya Marcelo Diaz wa Chile kulambwa kadi mbili za njano na kuwa nyekundu
dakika ya 28 kabla ya Marcos Rojo wa Argentina baadaye naye kutolewa nje kunako
dakika dakika ya 43 kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja.
Baada ya
kumalizika kwa muda wa dakika 120 ndipo ilipofikia hatua ya upigaji wa penati
ili kuamua bingwa mpya wa michuano hiyo maalumu ambayo imefanyika kwa mara ya
kwanza tena ikifanyika nje ya bara la Amerika ya Kusini nchini Marekani
ikishirikisha mataifa 16 kutoka mabara ya Amerika Kusini, Kaskazini na Kati na
Caribbean.
Katika zoezi
la upigaji wa penati, Chile ndiyo walioanza ambapo kiungo fundi mkabaji Arturo
Vidal alianza kwa kukosa mkwaju wake wa penati na baadaye mshambuliaji hatari
wa Argentina Lionel Messi na kiungo Lucas Biglia nao walikosa penati zao kwa
upande wa Argentina.
Hii inakuwa
fainali ya pili ndani ya miaka miwili kwa timu hizi mbili kukutana katika hatua
ya fainali ambapo mara zote mbili Chile wamechukuwa kikombe hicho kwa mikwaju
ya penalti.
Post a Comment