Bango la Taasisi ya Aziz Mahmud likiwa limefungwa eneo la machinjioni palikofanyika shughuli za uchinjaji. |
Mmoja wa wasimamizi wa shughuli za uchinjaji na mjumbe wa Taasisi ya Aziz, Bw. Hamad Al- Maamar akionesha ng'ombe 50 waliotolewa na taasisi yake kwa ajili ya kutolewa sadaka ya IDD EL HAJJ. |
Kazi ya uchinjaji na uchunaji ikiendelea eneo la machinjio Shinyanga mjini. |
Hapa baadhi ya viongozi wakiandika utaratibu wa usambazaji wa sadaka hiyo kwenda kwenye vituo mbalimbali mjini Shinyanga |
Moja ya gari kutoka kituo cha Mhumbu Islamic Shinyanga likiwa tayari kubeba msaada wa nyama kwenda kituoni. |
TAASISI
ya Aziz Mahmud Hudayi Wakf (Rehema Friendship and Solidarity Trust
(REFSO) yenye makazi yake jijini Dar es Salaam imetoa sadaka ya ng’ombe 50
wenye thamani ya shilingi milioni 30 kwa makundi mbalimbali ya watu wasio na
uwezo wakiwemo walemavu wa ngozi waliopo katika kituo cha Shule ya msingi
Buhangija Jumuishi Shinyanga.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa taasisi hiyo, Hussein Mohamed,
sadaka hiyo imetolewa ikiwa ni katika kuwakumbuka watu wasio na uwezo ili wa mjini Shinyanga nao
waweze kusherehekea vizuri siku kuu ya Idd el Hajj ambayo huambatana na sadaka
ya kuchinja.
“Huu
ni mwaka wa pili tumekuwa tukitoa sadaka hii katika baadhi ya mikoa hapa
nchini, lengo letu ni kuwasaidia watu wasio na uwezo waweze kupata kitoweo
katika siku kuu hii ya Idd el Hajj ambayo huadhimishwa na waumini wa kiislamu
ulimwenguni kote ikienda sambamba na sadaka ya kuchinja,”
“Kwa
hapa Shinyanga mwaka huu sadaka hii itatolewa kwa makundi mbalimbali ikiwemo
vituo vinavyotunza watoto yatima na kile cha Buhangija kwa watoto wenye ulemavu
wa ngozi (albinism), pia msaada kama huu umetolewa katika mikoa mingine nchini,” alieleza Mohamed.
Mbali
ya sadaka hiyo kupelekwa kwa makundi ya watu wasio na uwezo pia itatolewa kwa
waumini mbalimbali wa kiislamu waliopo kwenye misikiti ya mjini Shinyanga na
kwamba zaidi wa waumini 1,000 wanatarajiwa kupata sadaka hiyo ya EID EL HAJJ.
Septembar 24, 2015.
Post a Comment