Hapa Mukadam akiwa na mwenyekiti wa Kamati yake ya kampeni, Rashid Juma Mhango wakisubiri kutangazwa kwa matokeo katika kituo cha Tawi la CCM Nkomo. |
ALIYEKUWA Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Shinyanga, Gulam Hafeez Mukadam ameibuka na ushindi mkubwa katika kinyang’anyiro
cha kura maoni zilizofanyika katika kata yake ya Mjini Shinyanga.
Wasimamizi wa uchaguzi huo wa kura za maoni
ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika nchini kote Agosti mosi mwaka
huu, walimtangaza Mukadam kuwa mshindi katika uchaguzi huo baada ya kupata
jumla ya kura 247 katika matawi yote mawili ya kata ya mjini.
Mmoja wa wasimamizi wa kituo cha Tawi la Nkomo
mjini Shinyanga, Ibrahimu Ramadhani alisema katika kituo hicho Mukadam alipata
kura 182 akifuatiwa na mpinzani wake wa karibu Erasto Kwilasa aliyepata kura
53.
Mmoja wa wasimamizi wa uchaguzi katika kituo cha Tawi la CCM Nkomo, Ibrahimu Ramadhani akimtangaza rasmi Mukadam kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi huo wa kura za maoni. |
Wagombea wengine katika kituo hicho, Yusufu Mataba
alipata kura nane, Salumu Abdalah Zamzam kura mbili na Willy Mzava ambaye ni
mwenyekiti wa Umoja wa wazazi wa CCM mkoani Shinyanga aliambulia kura moja.
Katika kituo cha Tawi la CCM Mboya, aliyeongoza
alikuwa ni Erasto Kwilasa kwa kupata kura 99 akifuatiwa na Mukadam aliyepata
kura 65 huku wagombea Mzava akipata kura tano, Mataba kura mbili na Salum
Abdalah Zamzam aliambulia kura mbili.
Mukadam akiondoka katika kituo cha kupigia kura cha Tawi la CCM Nkomo, kulia kwake ni Sheikh wa wilaya ya Shinyanga, Sheikh Suleiman Kategile. |
Kutokana na matokeo hayo Mukadam ndiye mshindi
wa jumla katika mchakato huo wa kura za maoni ambapo baadhi ya wanachama wa CCM
wa kata ya Mjini waliwapongeza wasimamizi wa uchaguzi katika vituo vyote kwa
jinsi walivyoendesha uchaguzi huo kwa uhuru na haki na hivyo mshindi kupatikana
kwa haki.
Mara baada ya wasimamizi kumtangaza Mukadam kuwa ndiye mshindi wa jumla kwenye uchaguzi huo wa kura za maoni mamia ya wanachama wa CCM waliokuwa wakimuunga mkono mgombea huyo waliingia mitaani kwa shamra shamra kubwa wakishangilia kwa ushindi huo mnono.
Ni shamra shamra kwa kwenda mbele ni baada ya Mukadam kutangaza mshindi wa jumla katika uchaguzi wa kura za CCM udiwani kata ya Mjini Shinyanga |
Matokeo yaliyotangazwa katika kituo cha Tawi la
CCM Nkomo, Masele alipata jumla ya kura 191 akifuatiwa na Erasto Kwilasa
aliyepata kura 34, Hassan Fatiu (6), Charles Mlingwa (4), Abdalah Seni (4),
Willy Mzava (1) na Mussa Ngangale (5) huku wagombea wawili Tara Nzeimana na
Kazungu hawakuambulia hata kura moja.
Kituo cha Tawi la CCM
Mboya, Masele alipata kura 85, Kwilasa 69, Mlingwa (5), Fatiu (4), Nzeimana
(2), Mzava (8), Ngangale (4) Seni (5) na Kazungu hakuambulia kitu.
Kwa mujibu wa taarifa
kutoka katika baadhi ya kata mbalimbali ambazo hata hivyo hazijathibitishwa na
mamlaka husika, mgombea Masele alikuwa akiongozi kwa kura nyingi katika vituo
vyote vya kupigia kura.
Post a Comment