Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe.
Kuna maana mbaya sana ya CCM kuvunja makundi. Hii ina maana na mafisadi wote wanaingia kwenye mchakato na wameishahakikishiwa maslahi yao.


Kwa macho ya haraka haraka na uzembe wa kuchunguza watanzania wengi wamefikiri wamepata mkombozi wa matatizo sugu yanayoikabili serikali yao kama ufisadi rushwa na huduma mbovu za uma kwa kuwa magufuli atagombea kupita CCM.

Wamesahau CCM ni system. System iliyojaa wizi na hakuna aliye ndani mwenye uwezo wa kuibadili au kuigusa. Wamuulize Mwakyembe.

Labda tukumbushane.

Kikwete ameingia madarakani akiwa mzalendo kupindukia. watu wakiwa na matumaini ya kutosha. Yani wakati huo alikuwa waziri kwa miaka mingi tu.

Mkewe alikuwa mwalimu wa shule ya msingi tu anapokea laki mbili kwa mwezi mpaka Jk anaingia madarakani.

Riziwani alikuwa kaajiliwa na kampuni ya Masha aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani.

Kiujumla alikuwa mtu mwenye maisha ya kawaida, asiye na tamaa lakini ilimchukua miezi minne tu kuwekewa kucha kali na meno makali na kufundishwa kurarua. wakaivuta familia yake kwenye dili zao wakamziba mdomo. 

Baada ya hapo wakaanza kupiga mara Richmond mara Escrow na madini. Wakakwamisha mipango yake mizuri kama katiba mpya na kukuza democrasia. Ila JK ni mwanaume kasubutu kuwanyima kuwapa nchi moja kwa moja watesi wake.

Mnamkumbuka na Mkapa. Aliingia kama kiongozi masikini kabisa na mfuasi wa sera za mwalimu. Nae aligeuzwa kutoka kumiliki Land lover wakamshirikisha mkewe kwenye dili kubwa kubwa na kumpa hisa kwenye taasisi za kifedha. Mkapa kushtuka wakampa hadi mgodi wa makaa ya mawe. Baadae Jamaa wakafanya yao. Mara Rada Epa na Bot.

Walimzidi akili na mwinyi pia. Mzalendo aliyependwa na mwalimu. Wakamuundia zengwe mkewe Mama siti. Wakamfanya ashindwe kabisa kuendelea namikakati ya kusafisha utendaji mbovu wa secta za uma na sera zake za Fagio la chuma. Watu wakafanya yao.

Tusitegemee miujiza kwa magufuli. Labda akae na familia yake sasa. Awe tayari kufunga mkewe na watoto wake wakiingizwa kwenye dili. Kama alivyofanya raisi wa korea kaskazini aliyemnyonga mjomba wake na kumtupa kwenye shimo la simba.

Kwa CCM ilivyo hakuna wakuendesha nchi kwa weredi ata kama anaweredi kiasi gani.

CCM sasa imetutangulizia kondoo mbele huku akifatwa na kundi la mbwa mwitu wenye njaa hatari. Tuchukue tahadhari!!!!

Tulishasahau kilasiku tunasema tatizo ni mfumo. Tunatakiwa tuufumue mfumo tu basi ambao ni CCM.

Kumgeuza magufuli wataanza kumchangia pesa za kampeni watamwekea na za escrow humohumo. baadae wanafanya yao kwa uhuru. Watawazungukia watoto wake na ukoo wake. kama walivyomuuzia nyumba ya uma mdogo wake ili kumkata kauli alipokuwa wizara ya ardhi.

Ikumbukwe CCM imeishavunja makundi na Mafisadi wote watakuwa wamehakikishiwa usalama namaslahi yao na sasa wanaingia kwenye kampeni kwa miguu miwili. 

TUMEKWISHA.

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Asante kwa kutembelea mtandao huu

Post a Comment

 
Top