Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi mkoani Simiyu kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Magale Shibuda ametanganza rasmi kukihama chama hicho na hivi sasa amejiunnga na chama Tanzania Democratic Alliance (TADEA).


Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, ikiwemo ITV, Shibuda ametangaza kujiunga na TADEA akiwa huko Zanzibar ambapo muda mfupi baada ya kutangaza hatua yake hiyo aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho cha TADEA.

Haikuweza kufahamika mara moja iwapo mwanasiasa huyo machachari atagombea tena ubunge katika jimbo la Maswa Magharibi kwa tiketi ya chama chake hicho kipya aidha atabaki na jukumu la kukijenga na kukiimarisha chama hicho ili kiwe miongoni mwa vyama imara vya kisiasa hapa nchini.

Hii ni mara ya pili kwa Shibuda kuhama kutoka chama kimoja na kujiunga na chama kingine wakati wa vipindi vya kuelekea uchaguzi mkuu nchini, kwa mara ya kwanza mwaka 2010 alihama kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na CHADEMA baada ya kuchukizwa na kile alichodai mizengwe ndani ya CCM kiasi cha kuangushwa katika uchaguzi wa kura za maoni.

Kwa hivi sasa anahama CHADEMA na kujiunga na TADEA, tusubiri huenda akagombea tena ubunge ama kutangaza kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya TADEA.   Chama hiki kilichoanzishwa mwaka 1990 hakijawahi kupata mwakilishi ndani ya bunge la Jamhuri ya Muungano tangu kilipoanzishwa, huenda Shibuda akakiondolea mkosi huo.




Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Asante kwa kutembelea mtandao huu

Post a Comment

 
Top