Mama mmoja amedai kuwa yeye na marafiki zake
wawili walizuiliwa kuingia katika kilabu moja ya burudani kwa sababu
zinazodaiwa kuwa ni wanene sana na wenye sura mbaya.
Bi. Stacey Owen 33, alikuwa ametoka na marafiki
zake wawili kwa ajili ya kupata burudani wakati wa usiku siku ya jumamosi
alipokataliwa kuingia katika baa moja jijini Manchester kwa sababu ya unene
wake.
Stacey amesema wao walizuiwa huku watu wengine
wakiingia katika baa hiyo maarufu mjini humo,
Mama huyo sasa anataka kuombwa radhi na
wamiliki wa Baa hiyo lakini mpaka sasa amedai hajapata ujumbe wowote kutoka
kwao.
Anasema sio kwamba anajiona kwamba yeye ni
mrembo sana lakini kilichomshangaza ni uwepo wa ubaguzi huo miongoni mwa
wateja.
Source: BBC News
Post a Comment