MAFUTA YA MKATE YENYE JINA NUTELLA
Mahakama moja nchini Ufaransa imewazuia wazazi kumpatia jina la Nutella mtoto wao wa kike baada ya kubainika kuwa jina hilo litasababisha awe akizomewa kila mara sambamba na kuchokozwa.


Katika hali isiyokuwa ya kawaida Jaji wa mahakama hiyo badala yake aliagiza mtoto huyo apewe jina la Ella.

Alisema katika uamuzi wake kwamba jina Nutella ni jina linalotumiwa na mafuta yanayotumiwa kupaka mkate.

“Ni kinyume na maslahi ya mtoto ambapo jina hilo litamfanya kuchokozwa ama hata kuzomwa,'' alisema.

Wazazi nchini Ufaransa huwa wako huru kuchagua majina ya watoto wao , lakini viongozi wa mashtaka wana haki kuripoti kile wanachoona kuwa sio majina mazuri.

Wazazi wa kesi hiyo hawakuwasili mahakamani ili kusikiliza kesi yao ambapo  jaji huyo aliamuru kwamba jina Ella ndio jina zuri la kupewa msichana huyo.

Kumekuwa na msururu wa kesi zinazohusu majina ya watoto Ufaransa tangu mwaka 1993, wakati wazazi walipopewa uhuru  wa kuwapa majina wanayoyaka.

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Asante kwa kutembelea mtandao huu

Post a Comment

 
Top