Aliyeuawa Simanjiro katika mgogoro wa Madaraka ya CCM, azikwa
Mchungaji wa Kanisa la KKKT akiendesha misa ya mazishi Nurueli Mbaga |
Mgogoro wa kugombea madaraka ya uwenyekiti wa kijiji cha kambi ya chokaa
wilayani Simanjiro umeingia katika uvunjifu wa amani baada ya mmoja wa
wajumbe wa serikali ya kijiji anayemuunga mkono mgombea aliyependekezwa
na CCM Mbiki Ratoi Bwana Yohana Rometi kuuawa kwa kupigwa na vitu vyenye
ncha kali na wananchi wanaodaiwa kuunga mkono upande wa pili.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari mjumbe huyo
wa serikali ya kijiji ambaye anatajwa kumuunga mkono mgombea mmoja kati
ya wanaogombania nafasi hiyo anayedaiwa kuuawa na mashabiki wa upande
wa pili katika vurugu zilizofanyika kijjijini hapo na kushuhudia watu
waliojawa na huzuni huku wengine wakibubujikwa machozi baada ya mwili wa marehemu Yohana Rometi kuwasili
ukitokea hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza kifo hicho kaka wa marehemu Yohana Rometi Bwana John Rometi amesema tukio
ilo limewatisha na anashindwa kuamini kuwa watanzania sasa wamefikia
hatua ya kutoana uhai kwa ajili ya ushabiki wa kisiasa tena kwa chama
kimoja huku akiiomba serikali itende haki na mmoja wa viongozi wa
serikali ya kijiji hicho Kiberesa Kunei akiwataka familia ya marehemu
kutolipiza kisasi kwani wameshaikabidhi serikali ili iweze kuchukua hatua.
Akihubiri
katika ibada ya maziko mchungaji kiongozi wa kanisa la KKKT usharika wa Nomieuti wilaya ya Simanjiro Nurueli Mbaga amesema watanzania wa leo
wamekuwa wabaya kuliko wanyama kwani dhulma, uonevu na ukatili vimeshika
nafasi kuliko haki huku mwenyekiti aliyepitishwa na CCM anayedaiwa
kuungwa mkono na marehemu ambaye ameapishwa Desemba 29
mwaka jana Mbuki Molel Ratoi akiwasii wananchi kuacha visasi kwa kuwa
havina nafasi kwa sasa.
Post a Comment