MGOMBEA wa udiwani kata ya Malita Wilaya ya Maswa Mkoania Shinyanga Jeremiah Shigara anatuhumiwa kuiba nyara za serikali kinyume na sheria,
Shigara aliiba nyara hizo mali ya mbunge wa jimbo la Maswa anayemaliza muda wake John Shibuda katika mkutano wa wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika katika kata ya Malita Wilayani humo jana
Nyaraka hizo ni barua mbalimbali kutoka Wizara tofauti za serikali ambazo zilikuwa zimefungashwa kwa pamoja ambapo mbunge alikuwa akizitumia kujibia hoja na maswali ya wajumbe wa mkutano huo waliohitaji kufahamu utekelezaji wa ilani ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.
Shibuda alikuwa amempa kaimu mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo Mayenga Sangalali ambaye alikuwa akiongoza mkutano huo kwa kuondoa hofu kwa wajumbe kuwa alichokuwa akijibu ni sahihi na siyo mambo ya ubabaishaji.
Sangalali alipotakiwa na mbunge kurejesha nyaraka hizo alizikosa mezani, hata hivyo baaddhi ya viongozi wezake waliokuwa katika meza ya heshima walimweleza mwenyekiti huyo kuwa Shigara ndiye aliyezichukuwa nyaraka hizo na kutoweka katika eneo la mkutano.
Hata hivyo baadhi ya wajumbe wa mkutano huo waliomuona wakati akiondoka katika eneo la mkutano akiwa na nyaraka hizo walisema kuwa Shigara alisikika akisema “tuna shaka na barua hizi za mbunge huenda ni za kughushi ngoja nizipeleke usalama wa Taifa zikachunguzwe.”
Kutokana na kibwa kwa nyaraka hizo mwenyekiti huyo (Sangalali) amekwisha fungua kesi namba MAS/IR/689/2010, katika kituo cha Polisi cha wilaya ya Maswa na jeshi la polisi linaendelea kumsaka mtuhumiwa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Daud Siasi amethibitisha kutokea kwa wizi wa nyaraka za serikali na kuongeza kuwa mtuhumiwa atakapopatikana atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Mwisho.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Asante kwa kutembelea mtandao huu

Post a Comment

 
Top