Wadau wakisikiliza kwa umakini mkubwa maelezo ya awali juu ya uzinduzi wa Program ya Usawa wa Kijinsia kujenga uwezo wa kiuchumi kwa wanawake na Vijana.
 
Washiriki wa uzinduzi wa Program katika picha ya pamoja.
PROGRAM ya “Usawa wa Kijinsia kiuchumi kwa wanawake wa na vijana imezinduliwa rasmi mkoani Shinyanga itakayotekelezwa kwa kipindi cha miezi sita katika wilaya mbili za Shinyanga vijijini na Kishapu.
  
Lengo la program hiyo ni kujenga uwezo, uelewa na mikakati ya kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia.

Ofisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Muhoja akifungua rasmi uzinduzi wa Program kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,
Akitoa taarifa kwa wadau walioshiriki kwenye uzinduzi huo, Ofisa mradi kutoka Shirika la Kivulini lenye makao makuu yake jijini Mwanza, Eunice Mayengela amesema, program hiyo itatekelezwa katika vijiji vya Nyida, Nsalala, Welezo, Nduguti na Ihalo kata ya Nyida kwa wilaya ya Shinyanga vijijini.

Kwa upande wa wilaya ya Kishapu kata zitakazohusika ni Talaga, Shagihilu, Uchunga, Lagana na Negezi  katika vijiji vya Nhobola, Shagihilu, Ndoleleji, Unyanyembe, Kakola, Mwadulu, Lagana, Bulima, Negezi na Isoso.

Akifafanua Mayengela amesema Program hiyo itajikita katika kutoa mafunzo juu ya sera na sheria zinazoshughulikia masuala ya ukatili wa kijinsia kwa wawakilishi wa serikali za mitaa, polisi, na watoa huduma wa afya.

Pia patakuwepo na kampeni ya vyombo vya habari kuhusu sera, sheria na mafunzo iliyopo katika kutetea usawa wa kijinsia.

Kuanzisha, kujenga uwezo na kuimarisha mfumo wa rufaa wa kushughulikia mashauri ya ukatili wa kijinsia kati ya serikali za mitaa, jeshi la polisi, idara ya afya na mahakama.

"Pia tumelenga kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa njia ya midahalo na sinema, kutoa mafunzo kwa wanamabadiliko ngazi ya jamii (300) ili wafichue na kuchukua hatua za kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia katika maeneo yao," alieleza Mayengela.

MATOKEO TARAJIWA.

Alisema matokeo tarajiwa yanayotarajiwa baada ya kukamilika kwa program hiyo ya majaribio ni kuongeza uelewa kwa masikini na makundi maalumu kuhusiana na sheria, sera, na mifumo

MAONI YA WADAU.

Wadau katika ushauri wao walishauri, ni vizuri pia program hiyo ikiwashirikisha pia wanaume bila ya kuwabagua na kwamba iwapo utamaduni wa kumtetea zaidi mwanamke utaendelea kuwekewa mkazo ipo hatari katika miaka ijayo kuanzishwa kwa program nyingine ya itakayolenga kuwatetea wanaume.

Pia walielezea hofu yao kwamba iwapo walengwa wa masuala ya kupiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia watakuwa wanawake na watoto pekee, upo uwezekano wa ndoa nyingi kuvunjika baada ya wanaume kuhisi wanawake hawawajali.

Katika ufafanuzi uliotolewa na wawezeshaji kutoka Kivulini ilielezwa program hiyo haimaanishi imelenga kuwabagua wanaume bali itajikita katika utoaji wa elimu kwa watu wa jinsi zote mbili kwa lengo la kukomesha vitendo vya ukatili miongoni mwa jamii.

Ilifafanuliwa kuwa linapozungumzwa suala la jinsia halimlengi mwanamke au mwanamume pekee, bali linalenga makundi ya watu wote bila kujali jinsi zao ambapo pia ulitolewa ufafanuzi juu ya tofauti ya neno JINSIA na JINSI.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisa mradi kutoka KIVULINI, Eunice Mayengela alisema kutokana na mkoa wa Shinyanga kuwa miongoni mwa mikoa inayokabiliwa na kiwango kikubwa cha ukatili wa kijinsia ikiwemo mauaji ya vikongwe, Shirika la OXFAM kwa kushirikiana na Kivulini wamepanga kutekeleza program ya kuhamasisha, Usawa wa Kijinsia kujenga uwezo wa kiuchumi kwa wanawake na vijana.

"Kupitia Program hii, Kivulini inalenga kuongeza uelewa kwa jamii na serikali za mitaa katika usawa wa kijinsia, sera, sheria na matumizi ya mifumo inayohusiana na kuwasaidia wahanga wa ukatili,"

"Lakini pia kuwezesha serikali za mitaa kutambua wajibu wao katika utekelezaji wa sera na sheria zinazotetea usawa wa kijinsia katika kumkomboa mwanamke katika ukatili wa kijinsia," alieleza Mayengela.

Katika hatua nyingine wadau hao walijipangia mpango kazi wa jinsi watakavyoshirikiana na shirika la Kivulini katika kufanikisha utekelezaji wa Program hiyo katika maeneo yao.

TUMEKUWEKEA HAPA PICHA ZAIDI ZA MATUKIO YA UZINDUZI WA PROGRAM KWA WILAYA ZA SHINYANGA NA KISHAPU.

Wadau katika kikao cha uzinduzi wa Program.
Ofisa Miradi kutoka Shirika la Kivulini, Eunice Mayengela akiwasilisha kwa wadau mpango mzima wa jinsi program itakavyotekelezwa katika wilaya za Kishapu na Shinyanga vijijini.



Ofisa Miradi kutoka Shirika la Kivulini, Eunice Mayengela akiwasilisha kwa wadau mpango mzima wa jinsi program itakavyotekelezwa katika wilaya za Kishapu na Shinyanga vijijini.




Wadau wakifuatilia kwa umakini maelezo kuhusu utekelezwaji wa Program.

Mdau kutoka kijiji cha Nduguti kata ya Nyida wilayani Shinyanga, Saleh Manota akichangia hoja yake.



 
Groly Mlaki kutoka Shirika la Kivulini akisherehesha baadhi ya maelezo juu ya utekelezaji wa program pamoja na kujibu maswali yaliyoulizwa na wadau.




Baadhi ya wanahabari wakifuatilia uzinduzi kwa umakini.
 
Wana habari nao hawakuwa nyuma katika uchangiaji wa mada, Marco Maduhu kutoka gazeti la NIPASHE akitoa mchango wake wa mawazo. 

 WADAU WAKIPANGA MPANGO KAZI WA UTEKELEZAJI WA PROGRAM.
 







Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Asante kwa kutembelea mtandao huu

Post a Comment

 
Top